SELEMAN
Matola, Kocha wa Polisi Tanzania amesema kuwa kikosi chake kimetengamaa na
kitaleta ushindani kwenye ligi msimu ujao.
Polisi
Tanzania imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu na itakuwa miongoni mwa timu 20
ambazo zitashiriki ligi inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 juni ambapo itacheza na Coastal Union ya Tanga uwanja wa Ushirika Moshi.
“Tupo sawa
na kikosi chetu kina moto wa kutosha kabla ya ligi kuanza hivyo imani yetu ni
kufanya makubwa msimu utakapoanza hasa ukizingatia ni kikosi kipya lazima
wachezaji wawe na mambo mapya.
“Kwenye
ligi hatuna hofu iwe ni Coastal Union, Simba, Yanga,
Azam tutapambana, tunatambua kwamba ligi itakuwa ngumu nasi tutakaza," amesema.
Haya wasubirini Yanga muwatie virungu.....
ReplyDelete