ALMIN Kuc,
Meneja wa bondia Mserbia Scheka Gurdijeljac ambaye atashuka ulingoni kwenye
pambano la kimataifa litakalokuwa na raundi 12 la kimataifa dhidi ya Mtanzania
Bruno Tarimo, maarufu kama Vifua Viwili.
Pambano hilo
linatarajiwa kuchezwa Agosti 31 nchini Serbia ukumbi wa Hala Pendik Novi Pazar litakuwa ni la kukata na shoka.
Akizungumza
na Saleh Jembe Meneja wa Scheka ambaye ni bondia raia wa Serbia amesema kuwa
sababu kubwa ya kumchagua Vifua Viwili ni uwezo wake alionao pamoja na kiu ya
mafannikio iliyojificha kifuani mwake.
“Tumefanya
mawasiliano na Meneja wa Bruno kutokana na uwezo wake alionao kwenye boxer pia
ni mpambanaji ambaye uwezo wake unavutia akiwa ndani ya ulingo.
“Imani yetu
ni kuona pambano kali na la haki mshindi atapatikana bila ubaguzi kwani tunajua atatoa changamoto kubwa kwa bingwa
wetu, Scheka matumaini yetu kuona yule atakayepambana ndiye atakayeshinda,”
amesema Kuc.
0 COMMENTS:
Post a Comment