August 25, 2019


RASMI leo Simba imetolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye mchezo wa marudio uliochezwa uwanja wa Taifa.

Simba inatolewa na UD Songo kwa faida ya bao la ugenini ambalo wamelipata leo huku Simba wakiwa hawaamini wanachokiona.

Leo Simba walitakiwa kupata ushindi wa aina yoyote na kulinda bao lao mwisho wa siku walikubali kufungwa dakika ya 14 kwa uzembe wa mabeki ambao waliusindkiza kwa macho mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha wa UD Songo, Luis dakika ya 14.

Bao lao la usiku lilifungwa na Erasto Nyoni dakika ya 87 halikusaidia kuivusha hatua ya leo kutokana na kutokuwa na bao la faida walilopata kwenye mchezo wa kwanza.

Sasa Simba itaungana na KMC ambayo nayo ilitolewa uwanja wa Taifa kwa kufungwa mabao 2-1 na AS Kigali kuzipa sapoti timu mbili za Tanzania zilizosonga hatua ya mbele ambazo ni  Yanga pamoja na Azam FC.

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa haikuwa bahati yao leo kushinda kwani wamepoteza nafasi nyingi za wazi.

6 COMMENTS:

  1. Manula vipi goli jepesi mnooo

    ReplyDelete
  2. Simba hutolewaga katika wakat ambao huwez kuamini. Poleni sana Simba ila jitihadq kubwa mliionesha. Hakuna asiyeliona hili

    ReplyDelete
  3. Ndo mpira....hatuja fikia malengo yetu kilicho baki tuangalie makombe yaliyo baki t.....

    ReplyDelete
  4. UZEMBE HUO AMNA KITU HAPO WACHEZAJI WAZEMBE KABISA,KIPA HAJUI KUPANGA MABEKI NA NDIO MAGOLI ANAYOFUNGWA KILA SIKU,SHAME ON U WATU TUNASPEND HELA KUSAFIRI TOKA MKOANI AFU WACHEZAJI WANAZEMBEA,WACHEZAJI WALIJAA MAJIVUNO SANA KAMA WANACHEZA MPIRA NA ALLIANCE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siyo wachezaji tu hata mashabiki mlijaa mno majivuno utafikiri kwa kuwa msimu uliopita mlifika robo fainali hivi moja kwa moja safari hii mngeanzia nusu fainali kumbe la. Si vizuri kuwaita wenzenu chekechea wakati tayari wameshinda tena ugenini na hivi kuvuka hatua inayofuata, wakati nyinyi mkijiita Form six hata kabla ya kuingia uwanjani. Tujifunze kuweka akiba ya maneno!

      Delete
  5. Hayo ndo matokeo ya mpira siajabu sana ni kawaida tu kwani wote walitamani kusonga mbele YANGA msitucheke sana maana sisi ndo tumewapa nafasi ya kushiriki mashindano haya la sivyo msinge shiriki . Kazen mlinde nafasi ya team 4 Bongo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic