August 1, 2019

BAKARI Shime 'Mchawi Mweusi' Kocha Mkuu wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 'Tanzanite' amesema kuwa kesho watafanya kweli.

Tanzanite kwa sasa ipo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya COSAFA ambayo imeanza kutimua vumbi leo.

"Kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wamepewa majukumu kwa ajili ya mashindano haya ambayo tumealikwa hivyo ni muda wa watanzania kuwa na imani na sisi," amesema.

Leo kikosi kimefanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kwanza kesho dhidi ya Botswana utakaochezwa  Uwanja wa Gelvandale,Port Elizabeth,Afrika Kusini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic