SIMBA leo wametangaza kuingia mkataba mwingine na benki ya Equity ambao una malengo ya kusimamamia mradi wa kadi mpya za za wanachama na mashabiki zitakazoitwa Simba Card.
Kupitia ukurasa wa Instagram wameandika namna hii:-"Tumeingia mkataba na benki ya Equity ambao utawezesha benki hiyo kusimamia mradi wa kadi mpya za wanachama na mashabiki ambazo zitaitwa Simba Card.
"Kadi hizo zitatumiwa na wanachama na mashabiki kuweka akiba ya pesa na kutoa pindi wanapotaka kutumia, lakini pia kulipa ada ya kila mwaka, kununua tiketi za kuingia mpirani, na kupata punguzo la mpaka 10% kwenye maduka makubwa ambayo tutashirikiana nayo.
"Faida kubwa kwa klabu katika kadi hizo ni makato yanayopatikana wakati wa kufungua akaunti, kukusanya ada kisasa na mara moja kwa mwaka, na kupata takwimu sahihi za mashabiki iwapo kila shabiki atafungua akaunti.
"Kadi hizo zitaanza kutolewa Septemba mosi mwaka huu kwa kuwabadilishia kadi wanachama wa sasa na baadae litaendelea kwa wanachama wapya na mashabiki,",
Vyema....huo ndio mfumo wa kisasa..club nyingin zifuate njia h
ReplyDeleteThis is SIMBA....IGA UFE:This is next level.Vyura endeleeni kusubiria msumari wa moto kutoka kwa babu yenu Ninja na hawo komandoo njaa wanaongojea kupiga pesa za ada za wanachama na viingilio vya kuingia uwanjani maana sasa ni mwendo wa kidigitali tu.
ReplyDeleteHuu mpango kuboko hata mabenki yaliyozembea kuvuna wateja itabidi wahangaike sasa kutafuta wateja kwani wanachama na mashabiki wa Simba wametapakaa nchi zima. Aliyebuni huu mpango ni genius.
ReplyDeleteThis is next level brother.
ReplyDelete