UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unatambua ushindani utakavyokuwa Agosti 4, mbele ya kikosi cha Kariobangi Sharks ila wamejipanga kutoa burudani,
Dismas Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kwa sasa kila kitu kinakwenda sawa namaandalizi kwa wachezaji yapo sawa.
"Siku ya kilele cha siku Mwanachi itakuwa ni siku ya burudani ya kipekee na timu yetu inaendelea kufanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, mwinyi Zahera.
"Wapinzani wetu si watu wa mchezemchezo tunatambua ubora wao kwani Everton walinyoosha mikono kwao hivyo nasi tuna kazi kubwa ya kufanya, pia walifanya vizuri kwenye michuano ya SportPesa.
"Wito wangu kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi kuona namna tutavyotoa burudani kwani kuhusu vifaa na jezi zote halisi zitakuwepo pamoja na mpango mzima wa kuwatambulisha wachezaji wetu," amesema.
Everton na Kariobangi zilicheza mchezo wa kirafiki dakika 90 zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na kupelekea kupigwa penalti ambapo Kariobangi ilishinda penalti 4-3

0 COMMENTS:
Post a Comment