August 21, 2019


Raarifa zimeeleza kuwa Edward amemalizana na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa kusaini mkataba wa miaka minne itakayomfanya aendelee kuhudumu mpaka mwaka 2023.

Maka ameondoka Yanga akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na aliondoka nchini mwezi Juni kuelekea Latvia kwa madhumuni ya kufanya majaribio na Spartaks Jurmala.

Baada ya kumaliza majaribio hayo, Maka alirejea nchini lakini leo ameibukia tena Morocco akiwa na timu hiyo mpya.

Inaelezwa kuwa majaribio aliyoyafanya Maka na Spartaks yalimsaidia kuweza kumalizana na Atheletico waliokuwa wakimfuatilia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic