STRAIKA MPYA SIMBA AWAITA MASHABIKI UWANJA WA UHURU
Mshambuliaji wa Simba, Deo Kanda ambaye amesajiliwa kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea TP Mazembe ya DR Congo, amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna watakavyotoa burudani.
Simba inatarajiwa kukipiga dhidi ya Mtibwa Sugar, leo Ijumaa katika mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu Bara wakiwa wao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo ambapo mchezo utapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kanda alisema anaona kikosi cha Simba kipo vizuri na wachezaji wanaelewana jambo ambalo linaipa nafasi timu yake kushinda.
“Wachezaji tunaongea lugha moja ambayo ni kutafuta ushindi, tuna nafasi ya kufanya vizuri, nawaomba mashabiki watupe sapoti na wajitokeze kwa wingi waone vitu tutakavyofanya,” alisema Kanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment