Mshambuliaji Mtanzania, Shiza Kichuya, anayekipiga katika timu ya Ligi Daraja la Kwanza Misri, Pharco FC, amesema mpaka sasa amehusika katika michezo sita ambayo timu hiyo imecheza ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya utakaoanza wiki ijayo.
Kichuya ambaye alijiunga na timu hiyo kwa kusaini mkataba wa miaka minne, ameeleza kuwa ndani ya mechi hizo sita tayari ameshaingia kambani mara mbili.
Kichuya amefunguka akieleza licha ya kufunga mabao mawili, pia amekuwa akipata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi na Kocha wake akifurahishwa naye.
"Mimi huku naendelea vizuri kwakweli, tunajiandaa na msimu mpya hivi sasa na tayari tumeshacheza jumla ya mechi za maandalizi.
"Katika mechi hizo sita nimefanikiwa kufunga mabao mawili kwenye michezo tofauti na Mwalimu anafurahia maendeleo yangu, namshsukuru Mungu.
"Mazingira kwa huku nimeshazoea kwakweli, nishakuwa mwenyeji na nishazoeana na wachezaji wenzangu, changamoto zilikuwepo mwanzoni wakati naenda kwa mkopo ENPPI", alisema Kichuya.
Ikumbukwe Kichuya kabla hajajiunga na Pharco, mshambuliaji huyo alipelekwa ENPPI inayoshiriki Ligi Kuu Misri na baada ya kumalizika muda wake sasa amerejea Pharco alikosajiliwa kuanza kazi.
Mwanangu huko uliko daraja la kwanza ndio kutamu katika kujijenga kwa mchezaji mwenye kujielewa na uchu wa mafanikio.
ReplyDelete