September 15, 2019


Kiungo wa Simba, Jonas Mkude amesema sasa ndani ya timu hiyo ni raha kwani ameanza kuelewana vyema na kiungo mwenzake, Sharaf Eldin Shiboub raia wa Sudan.

Mkude alisema kuwa kwa sasa uelewano wao ndani ya uwanja umeongezeka kwa hiyo anaamini kabisa kadiri siku zinavyoenda mambo yatakuwa makubwa zaidi ya ilivyo sasa.

Alisema Shiboub ni moto wa kuotea mbali kutokana na aina ya uchezaji wake kwa hiyo wanapokuwa uwanjani wote kila mmoja sasa anajua nini mwezake anatakiwa kufaya wakati akiwa na mpira na nini anachotakiwa kufanya akiwa hana mpira.

“Kwa hiyo, niwaambie tu mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi lazima tuchukue ubingwa kwa mara nyingine tena.

“Kwa jinsi mambo yalivyo sasa naamini hakuna wa kutuzuia, uelewano wangu wa Shiboub uwanjani umeongezeka sana,” alisema Mkude.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic