ABDU KIBA AJIBU MADAI YA NDOA YA KAKA YAKE KUVUNJIKA
Baada ya ndoa yake na ya kaka yake, Ally Kiba kudaiwa kuvunjika, mwanamuziki Abdul Kiba ‘Abdu’ ameibuka na kujibu madai hayo ambayo yametawala kila kona.
Awali, habari zilisambaa kuwa wanamuziki hao ndoa zao zimevunjika na katika kulithibitisha hilo ni hivi karibuni baada ya Abdu Kiba kumfanyia mwanaye sherehe ya bethidei nyumbani kwa kaka yake lakini wake zao hawakuonekana.
Habari hizo zilizidi kueleza kuwa, kwenye sherehe hiyo ya mtoto wa Abdu Kiba ambaye amezaa na mwanamke mwingine (siyo mke wa ndoa) ilifanyika Tabata, Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki tu lakini wake wa wawili hao hawakuwepo jambo ambalo lilizua gumzo na kuelezwa kuwa walishaachana.
Mtoa habari alidai kuwa kwa mujibu wa watu wa karibu ni kwamba ndoa hizo zimeshavunjika ila wasanii hao wamekuwa wakifanya kuwa siri kubwa, hawataki watu waujue ukweli.
ABDU AJIBU
Ili kuujua ukweli kuhusu habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Abdu Kiba ambaye alisema siyo za kweli kwani bado yeye na kaka yake wako kwenye ndoa zao.
Alipoulizwa kuhusiana na wake zao kutohudhuria sherehe ya bethidei ya mwanaye iliyofanyika hivi karibuni na wanafamilia wote kuwepo isipokuwa wake zao hao, Abdu Kiba alisema ni kweli hawakuwepo kwa sababu walikuwa wamesafiri.
“Ni kweli wake zetu hawakuwepo kwenye sherehe ya bethidei ya mwanangu, mke wangu amesafiri yupo Zanzibar na mke wa Ally kwa wiki tatu sasa yupo Kenya kwa hiyo ndoa zenu hazina tatizo lolote kama watu wanavyosema,” alisema Abdu Kiba.
April, 2018 Kiba alifunga ndoa na Amina Rikesh, raia wa Kenya na mpaka sasa wamejaliwa mtoto mmoja huku Abdu akifunga ndoa mwezi huohuo na Rwahida ambapo walifanya sherehe ya pamoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment