MZEE AKILIMALI ATOA UTABIRI WAKE, YANGA VS ZESCO
Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kuwa, ana uhakika wa timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa mabao si chini ya matatu watakapocheza dhidi ya Zesco ya Zambia, kesho Jumamosi.
Kauli ya Mzee Akilimali inakuja wakati Yanga ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa Zesco katika mchezo wa kwanza wa Hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa kwenye Uwanja Mzee Dar es Salaam wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mzee Akilimali ameliambia Championi Ijumaa kuwa: “Tayari nimeshaona tuna uwezo mkubwa wa kumfunga Zesco hapa nyumbani.
“Kuna kijana wangu ambaye alifanya mambo katika mechi iliyopita dhidi ya Township Rollers, ndiye aliyeniambia kwamba pia Zesco tutawatoa, tena kazi inamalizika hapa nyumbani.
Mzee unataka makubwa. Mukipata droo au moja basi mshukuru Myngun
ReplyDelete