UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utatoa zawadi za kutosha kwa mashabiki watakaoibuka uwanja wa Chamazi Jumapili kushuhudia mchezo wa kimataifa dhidi ya Triangle United ya Zimbabwe.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa Jumapili itakuwa ni siku ya kazi kwa wachezaji wa Azam FC kimataifa huku mashabiki wakipata burudani ya kutosha.
"Tumejipanga kwa ajili ya mashabiki wetu kuwapa burudani na furaha pale watakapokuja uwanjani hivyo ni muhimu kwao kutambua kwamba tunawajali wajitokeze kwa wingi kwani kuna zawadi nyingi juu yao.
"Kila shabiki atakayekuja kuishangilia Azam FC atapewa ukwaju pamoja na juice mpya ya ukwaju bure kabisa na kiingilio ni cha kawadia tu kwani kawaidia ni shilingi elfu tatu," amesema Maganga.
Mchezo wa marudio dhidi ya Triangle FC unatarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 27 nchini Zimbabwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment