September 7, 2019


Mechi ya kirafiki baina ya Yanga na Pamba SC imemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 1-1.

Mechi hiyo kwa Yanga imekuwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United Agosti 14 mwaka huu.

Bao la Pamba limefungwa mnmao dakika ya 30 kupitia kwa Saad Kapanga kwa shuti moja kali ambalo lilimshinda nguvu kipa Ramadhan Kabwili.

Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Yanga wakionesha juhudu za kusaka bao la kusawazisha lakini jitihada zao zilikuwa zinakwama kutokana na mabeki wa Pamba kuonesha umaridadi kwenye safu ya ulinzi.

Lakini katika dakika ya 90, David Molinga 'Falcao' aliyepata nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia, alipata nafasi nzuri na kuitumia vema akifunga bao la kusawazisha akimalizia pasi ya Deus Kaseke.

Bao hilo kutoka kwa Falcao linakuwa la kwanza kwake tangu asajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria.

2 COMMENTS:

  1. USHAURI NI KWA NAMNA IPI FURAHA IPATIKANE NA USHINDI URUDI YANGA

    1. TIMU KUIMPROVE UWEZO, MBINU NA KUSHINDA MECHI......JUKUMU BENCHI LA UFUNDI
    Nilisema hapo mwanzoni na narudia kusema kwa nia ya kujenga....hili mashabiki wahudhurie viwanjani bila kuwashurutisha ama kuwajengea hamasa ni lazima timu iweze kucheza soka la kuvutia na kuwa na mbinu za uwanjani kuweza kupata matokeo mazuri kila mechi....kuna mapungufu kwenye benchi la ufundi, wachezaji na mipango ya mazoezi na mbinu kwa ujumla....inawezekana uwezo wa ufundishaji ukawa umefikia ukomo....hili linahitaji mjadala na utatuzi haraka sana kabla ya mambo hayajaenda kombo.
    2. Mwalimu apunguze exposure (kujianika anika) kwenye vyombo vya habari na matukio mengi (harambee, mialiko ya kuonekana katika umati wa mashabiki, sikukuu za ufunguzi wa matawi, vipindi cha mahojiano na vyombo vya habari nk..) Ajikite zaidi kwenye fani yake ya kufundisha mpira....kifupi aishi ki-professional
    3. Hii dhana ya kwamba timu ya wananchi...isipoangaliwa inaweza ikaleta dosari na kuruhusu maadui kuingilia misafara ya timu na kudhuru timu kwa njia mbalimbali.....lazima kuwepo na udhibiti kwenye kambi na mazoezini na hata kwenye mechi....msiruhusuruhusu hata wanaokuja kwa lengo la mahojiano na vyombo vya habari hili suala libaki kuwa jukumu la uongozi (Mratibu wa Timu au Meneja)
    4. Wachezaji wawe na umoja na upendo 
    wenyewe kwa wenyewe na kuhimizana kucheza kwa ari na ushirikiano kwa manufaa ya timu...kushambulia kwa akili, mbinu na malengo sio kubutuabutua bora liende mbele.....viungo na mabeki kukaba bila kujisahau na kupunguza makosa makosa kwenye mechi....wachezaji kushirikiana kupunguza mianya ya makosa
    5. Suala la Mwalimu Msaidizi ili kulipa nguvu benchi la ufundi na kuimprove performance ya timu (kwani ni dhahiri uwezo wa timu na mchezaji mmojammoja unashuka kwa kasi mno).....Hata kama 2/3 ya timu ni wapya....lakini haionekani improvement ya kucheza kitimu...

    Ahsante

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic