LEO Uwanja wa Uhuru, timu ya Simba itawakaribisha Mtibwa Sugar ikiwa ni mchezo wa pili kwa kila timu kucheza msimu huu mpya wa 2019/20.
Kwa mujibu wa ripoti za timu zote mbili inaonesha kwamba jumla ya wachezaji watano wataukosa mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
Kwa upande wa Simba wenyewe ina wachezaji wawili majeruhi ambao ni pamoja na nahodha John Bocco anayesumbuliwa na goti pamoja na Mbrazil, Wilker da Silver naye anasumbuliwa na goti.
Kwa upande wa Mtibwa Sugar, nahodha Shaban Nditi, Salum Kihimbwa na Saley Hamis wataokusa mchezo wa kesho.
0 COMMENTS:
Post a Comment