Mshambuliaji wa Yanga, David Molinga ‘Falcao’ raia wa DR Congo amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwataka watulie kuwa mambo mazuri yanakuja kikosini hapo kutokana na kujipanga kutupia msimu huu.
Molinga ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa katika kikosi hicho msimu huu ambapo hadi sasa ameshatupia mabao matatu katika kikosi hicho ikiwa ni dhidi ya Pamba na Toto African.
Akizungumza kupitia ukalimani wa Pappy Tshishimbi, Molinga aliyekuwa akizungumza Kilingala alisema kuwa, amejipanga kuona anawapatia mashabiki wa Yanga kile wanachokihitaji kwa kuwafurahisha kwa kutupia mabao hivyo ameomba wamuamini.
“Nimekuja Yanga kwa kuchelewa kujiunga, lakini mwalimu ameweza kunitumia na kuniamini hivyo nashukuru Mungu, nimeweza kuonyesha uwezo na kufunga, nimefurahi kufanikiwa kufunga katika mechi hizi.
“Naomba mashabiki waniamini na mimi nitaonyesha uwezo zaidi nitafunga ili niwafurahishe,” alisema Molinga.
Naye Mratibu wa Yanga, Hafidhi Saleh alisema, kikosi hicho kipo vizuri na hakuna majeruhi hata mmoja isipokuwa Juma Mahadhi ambaye ni majeruhi wa muda mrefu.
0 COMMENTS:
Post a Comment