September 13, 2019


Kikosi cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara leo.

Ushindi huo umepatika kupitia mabao ya Meddie Kagere dakika ya 17 kipindi cha kwanza na Miraji Athumani akifunga dakika ya 68 kipindi cha pili.

Kabla ya Miraji kuongeza bao la pili, kipindi cha kwanza Riffat Khamis aliisawazishia Mtibwa dakika ya 20 ikiwa ni dakika tatu pekee Kagere acheke na nyavu na matokeo kuwa 1-1.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Simba walikuwa na mabao mawili huku Mtibwa wakiwa na moja.

Ushindi huo umewafanya Simba kufikisha jumla ya alama sita wakiwa kileleni mwa ligi.

Wakati huo, KMC nao waliokuwa ugenini Mkwakwani Tanga kucheza dhidi ya Coastal union wamelala kwa mabao 2-0 kutoka kwa Wagosi hao wa Kaya.

2 COMMENTS:

  1. Kocha wa Simba ana matatizo. Tatizo lake moja kubwa ni yeye mwenyewe binafsi kukosa kujiamini. Kwa kikosi cha Simba kilivyo nisingetarajia kusikia kocha akilia kuwa ana upungufu wa washambuliaji.Akili yake imeoza kwa wachezaji fulani wakati Simba tayari inamaingizo mapya ya wachezaji wa maana kabisa. Mfano Salum shamte alieotoka lipuli kwa ufahamu wangu mimi nafahamu kuwa ni mchezaji wa kiungo kabla hajaondoka simba hapo awali na alikuwa yupo vizuri kwenye nafasi hiyo. Khassan Dilunga sio winga peke yake bali anaweza kutumika kama mshambuliaji wa kati na akafanya maajabu.kocha wa Simba nakosa ujasiri wa kuwaamini baadhi ya wachezaji wake katika majukumu tofauti na siku zote nasema ni kitendo kinachowaondoshea kujiamini kwa wachezaji wake pia. Miraji Athumani? vipi kocha anakwenda kulia kuwa hana straika wakati anamchezaji kama Miraji Athumani? Binafsi naona kama Miraji ataaminiwa kikamilifu Simba basi watamsahau Okwii. Hata tatizo la ufungaji ndani ya Taifa stars naamini Miraji Athumani ndio suluhusho sahihi.Na ni kutokana na aina ya magoli yake ambayo anafunga hata tangu akiwa Lipuli ni magoli magumu.Ni magoli ya jitihada za mchezaji binafsi zaidi.Ni magoli ya kuamua mechi na ameshafanya hivyo sio mara moja.Goli lake kwa mtibwa sugar alifunga ndani ya kichaka cha mabeki hata kipa wa mtibwa Kado hakufikiria kama Miraji angekuwa na usubutu na ujasiri wa kufunga bao lile mbele ya mabeki. Sasa lakini utaona kocha wa Simba bado analilia mafowadi hata wakiwa peke yao na nyavu wanakosa magoli?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naunga hoja kwa asilimia mia.kocha aache kukariri wachezaji.Tunaona jinsi centre back mbrazil Traione Santos anavyocheza kwa utulivu na akili kuliko Wawa anayecheza mpira wa nguvu na hana utulivu na kupenda kulaumu wenzake.Nawashangaa makocha Aussems na mwenzake Denis Kitambi kwa mini hawachezi hata dk 15-20 kina Mpilipili,Ndemla,Kennedy wilson? Ukiangalia game nyingi za Simba formation wanayocheza ni za pasi nyingi na za kudokoa hadi waingie ndani ya penati box.Timu nyingi pinzani ni kama wameshaisoma vizuri Simba inavocheza hivyo unakuta muda mwingi timu pinzani wanapaki bus na ukweli rejea takwimu zote za game alizocheza Simba utaona possession hadi FT wakati wote wana asilimia kubwa na Mara nyingi zaidi ya asilimia 60 na wakiishia na ushindi wa magoli kiduchu.Hii itawapa taabu kwenye viwanja vya mikoani kama mocha hatabadili mifumo na kucheza wachezaji engine kama Ndemla ambaye Mara hufumua mashuti ya nguvu on target tokea mbali.Wenye ukaribu na bench hili la ufundi wafikishe ujumbe huu.Sitashangaa hata timu kama Mashujaa zikituhenyesha kwani ukweli timu nyingi zinafanya marejesho kwenye video game alizocheza Simba.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic