September 29, 2019


BAADA ya kikosi cha Yanga kupoteza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya Zesco United sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye Kombe la Shirikisho.

Yanga ilitolewa na Zesco kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2 hivyo wanafungasha virago kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na kutupwa kwenye Kombe la Shirikisho.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa haikuwa malengo ya Yanga kufikia hatua hiyo ila ni matokeo haina budi kuyapokea.

"Kwa sasa sisi ni wa kimataifa, kushindwa kwetu kutinga hatua ya makundi haina maana ya mwisho wa mbio kimataifa bali tunaingia kwenye Kombe la Shirikisho huko tutapambana.

"Shukrani kwa mashabiki kwa sapoti kubwa na Yanga tumeonyesha maana ya kuwa wa kimataifa tumetoka kulia tumeingia upande wa kushoto," amesema.

7 COMMENTS:

  1. Yanga Igepinduwa meza Tena kwa magoli mengi lakini imefungwa kutokana na hujuma waliyofanyiwa kwa kuzimiwa taa kama ilivotangazwa hapo mwanzoni

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha ha mfa maji.....walizimiwa taa uwanjani au?kwani mpira ulichezwa usiku?na kama ulichezwa usiku kwani hao zesco walikua na tochi?find another point brother that is nothing you wrote.

    ReplyDelete
  3. Sijaona msemaji aliposema "wamezimiwa taa!" Nimeona akiwashukuru mashabiki kwa kuiunga mkono timu na kusisitiza bado ni wa kimataifa. Full stop

    ReplyDelete
  4. bado hawajaingia makundi shirikisho..Wana mechi moja wakishinda hapo ndio wataingia makundi.Sasa inakuwaje bado wako sana kimataifa.Waje wamalizie viporo vyao na iwe kama ile ya Simba kila saa 72 mechi.. Wajue tayari walishafungwa na timu mbili za ligi kuu Polisi na Ruvu shooting

    ReplyDelete
  5. Vipi wangeuona mpira ilhali walizimiwa taa. Wamefanyiwa umafia

    ReplyDelete
  6. Wanalalamika wana tatizo la washambuliaji wakati Makame amefunga bonge ls GOLI .Linaweza kuwa goli bora la msimu .Visingizio tulitaraji walizimiwa taa wakashindwa kuona meza wakapindua stuli.Kelele nyingi mpira wenyewe hata kupiga pasi mbili shida.

    ReplyDelete
  7. muwe mnaweka akiba ya maneno. ndio maana mwafrika kuendelea tupo bado sana.
    eti yanga kupiga pasi mbili ilikuwa mtihan,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic