September 29, 2019



SIMBA ambao ni mabingwa wa watetezi wa Ligi Kuu Bara wameweka rekodi yao msimu huu mpya kwa kushinda mechi zote tatu walizocheza mpaka sasa.

Simba ilifungua ligi kwa kuanza kucheza na JKT Tanzania ambapo ilishinda kwa mabao 3-1 uwanja wa Uhuru.

 Mchezo wa pili uliopigwa tena uwanja wa Uhuru Simba ilishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na mchezo wa tatu ilishinda kwa mabao 3-0 mbele ya Kagera Sugar.

Ndani ya dakika 270 Simba imefunga jumla ya mabao nane huku ikiruhusu kufungwa mabao 2 na mlinda mlango Aishi Manula ana clean sheet moja aliyoipata mbele ya Kagera Sugar.

Mpaka sasa viungo wa Simba, Sharaf Shiboub na Mzamiru Yassin wote wametoa jumla ya pasi za mwisho nne huku kila mmoja akitoa pasi moja za mabao ndani ya Simba.

Kwa sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi tisa na leo itakuwa uwanja wa Karume kucheza na Biashara United ya Mara.

Kinara wa kucheka na nyavu ni Meddie Kagere ambaye naye amefunga jumla ya mabao matano na ametoa pasi za mwisho mbili.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic