September 11, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amemlipia Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali, kiasi cha shilingi za Kitanzania 369,000 alizokuwa anadaiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Zahera amemlipia Akilimali fedha hizo zilizotokana na kufanyiwa matibabu katika hospitali hiyo baada ya kuomba msaada kwa wadau mbalimbali ili wamchangie.

Akilimali amesema Zahera ameamua kumsaidia baada ya kupata taarifa zake kupitia Gazeti la Spoti Xtra ambalo hutoka kila Alhamisi na Jumapili na linachapishwa na Global Group.

Akilimali ameeleza kuwa Zahera aliguswa alipoona taarifa hiyo na kuamua kujitoa kumlipia fedha zote hizo huku akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya Global Group kwa mchango wake kwake.

“Ni kweli Zahera amenilipia deni lote ambalo ni Sh 369,000 na nimeshalipa tayari, sidaiwi tena.

“Aliona taarifa kupitia gazeti lenu la Spoti Xtra na akaguswa hivyo akaamua kunisaidia, kwa kweli nawashukuru sana Global kwa mchango wenu, mmenisaidia.

“Siwezi kuwa mchoyo wa fadhila kumshukuru sana Zahera, ameonesha ni mtu wa watu ukiachana na masuala ya mpira, pia shukrani kwa baadhi ya wadau wengine waliojitoa kunichangia,” alisema Akilimali.

Akilimali amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu ambao umekuwa ukisababisha hali yake kiafya kutokuwa nzuri.

Ikumbukwe kabla ya Zahera kumlipia deni hilo, mpaka kufikia Jumatano ya wiki iliyopita Akilimali alikuwa ameshapokea zaidi ya shilingi 34,000 ambazo alikuwa akitumiwa na wadau walioguswa na tatizo lake.

CHANZO: SPOTI XTRA

3 COMMENTS:

  1. Welldone Zahera umefanya kitu cha kiungwana sana.

    ReplyDelete
  2. Angemwacha akome na maneno yake ya kuchafua YANGA

    ReplyDelete
  3. Mungu amekuponya mzee, nilidhani upo vizuri kifedha kumbe....sasa ninaamini kumbe wazee wa simba na yanga wapo kimasilahi zaidi. Hata yule wa simba ndiyo maana alikatalia ile hati, siku hizi yupo kimya labda ameimgia kwenye kundi au wammp kitu kidogo. Tunashukuru mmelea vizuri hizi timu zetu za simba na yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic