KOCHA SIMBA AANZA KULALAMIKA, AFUNGUKA JUU YA UHITAJI WA MBADALA WA OKWI
Kocha wa klabu ya Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa safu yake ya ushambuliaji ina mapungufu na anahitaji asajiliwe straika mwingine.
Kauli hiyo imekuja kufuatia kuumia kwa nahodha wa timu hiyo, John Bocco, ambaye tayari ameshaanza mazoezi mepesi na wenzake sambamba na kuondoka kwa straika Mganda, Emmanuel Okwi.
Aussems ameeleza kwa namna anavyokiona kikosi cha Simba hivi sasa pale mbele anakiri wazi kuwa kuna mapungufu na inapaswa kufanyiwe marekebisho haraka.
"Ninahitaji straika ambaye ataleta changamoto kwenye safu ya mbele.
"Bado mpaka sasa sijaona kile ambacho nakihitaji kwani kuna changamoto kadhaa.
Wakati akiongelea udhaifu wa nafasi yake ya ushambuliaji, Aussems Ijumaa hii atakuwa ana kibarua kingine cha mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Ijumaa hii.
0 COMMENTS:
Post a Comment