October 15, 2019


Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, ana imani kubwa na kiungo wake mshambuliaji, Ibrahim Ajibu baada ya kurejea kikosini hivi karibuni akitokea kwenye majeraha.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari FC ya nchini Kenya uliopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliomalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 lililofungwa na kiungo huyo fundi.

Ajibu hadi hivi sasa amecheza michezo miwili ya Ligi Kuu Bara kati ya minne huku akitengeneza nafasi moja pekee ya bao lililofungwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere.

Aussems alisema kuwa kiungo huyo ameshindwa kuonyesha uwezo wake kwenye michezo miwili ya ligi kutokana na kutokuwa na ‘pre season’ nzuri kwake baada ya kupata majeraha.

Aussems alisema kiungo huyo tayari ameanza kurejesha fitinesi yake huku akiamini kwenye michezo ijayo atazidi kuonyesha kiwango kikubwa zaidi ya alichokionyesha walipocheza michezo ya ligi na Kagera Sugar, Biashara FC na huo wa Bandari.

“Maswali napokea kuhusiana na kiwango cha Ajibu, labda niwaambie ni kati ya viungo bora wenye uwezo wa kuchezesha timu na kubadili matokeo ndani ya dakika 90.

“Kikubwa Kilichosababisha ashindwe kuonyesha ubora wake ni majeraha yaliyomuwekea nje ya uwanja kwa muda mrefu na kusababisha kutokuwa na ‘pre season’ nzuri kwake.

“Na hiyo ilisababisha kukosa michezo miwili ya awali ya ligi, hivyo ninaamini kadiri atakavyokuwa anacheza mechi za ligi, basi atazidi kubadilika na kuonyesha kiwango kikubwa,” alisema Aussems.

3 COMMENTS:

  1. Ila baadhi ya serikali zetu za mikoa zinatia kichefuchefu.Nimeangalia uwanja ambao Simba wameutumia na mechi yake zidi ya Mashujaa kwa kweli ni kituko na aibu. Hapana shaka ule ni uwanja bora zaidi kuliko yote mkoani kigoma? Kwani uwanja wa mpira ni kitu gani jamani? Angalau kajiuwanja kamoja chenye muenekano mzuri mko mzima inashindikana? Angalau sehemu ya kuchezea iwe sawa achana na majukwaa. Kweli mpaka asubiriwe Magufuli? Kwakweli watanzania huwa tunajidumaza mno wakati mwengine kwa kusubiri kila kitu kufanyiwa. Kwa wenzetu suala la kupendezesha mazingira ni suala ambalo mara nyingi lisilohitaji mamilioni ya pesa bali linahitaji zaidi watu kujitoa kwani hata kama sehemu itajengwa miundo mbinu bora bila kuwepo watu wa kuitunza na kuiendeleza ni kazi bure. Viwanja vya mpira na maeneo ya wazi ni mapambo ya miji na yapendezesha miji kama yataandaliwa katika ya usafi na ubunifu lakini inaonekana Tanzania bado kabisa tumeshindwa kuyaboresha maeneo hayo ili yawe yanavutia.

    ReplyDelete
  2. Kumbuka ule uwanja unamilikiwa na chama chama pinduz so mkoa hauna chake pale

    ReplyDelete
  3. Tatizo no CCM inalazimisha kuvimiliki viwanja wasivyo miliki kihalali.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic