VITA ya ndani ya uwanja ni kupata pointi
tatu kwa kila mchezaji huku nyota anayeibeba timu ni yule anayecheka na nyavu
kwa kutimiza majukumu yake ndani ya timu.
Kwenye kila msimu wa ligi huwa kunakuwa
na mfumania nyavu bora ambaye yeye hupewa tuzo ya heshima kwa kile
alichokifanya hata kama timu yake itashindwa kutwaa ubingwa.
Kwa muda wa misimu 10 rekodi za
watupiaji nyavu kwenye Ligi Kuu Bara ilikuwa inaishia kwenye idadi ya mabao 20
na yule aliyejitutumua sana aliishia 21, hiyo ilikuwa kuanzia msimu wa mwaka
2004, ni mfungaji mmoja tu aliyetupia jumla ya mabao 23 huyu si mwingine ni
Meddie Kagere anayekipiga Simba.
Hizi hapa rekodi alizozipoteza kwa
wafumania nyavu ndani ya ligi walioibuka wababe wa tuzo ya ufungaji bora ndani
ya Bongo.
2008/09
2008/09
Boniphace Ambani wa Yanga nyota huyu alikuwa
mkali wa kucheka na nyavu akiwa kwenye ubora wake licha ya umri kumtupa mkono
alimaliza msimu akiwa amecheka na nyavu mara 18.
2009/10
2009/10
Mussa Mgosi, mshambuliaji
wa Simba, kwa sasa yeye amepewa majukumu ya kuwa kocha kweye timu za vijana
ndani ya Simba pamoja na ile ya Simba Queens, yeye alitupia jumla ya mabao 18
na kutwaa tuzo ya ufungaji bora.
2010/11
2010/11
Tuzo ilibebwa na Mrisho Ngassa, ukimwita uncle utakuwa hujakosea, msimu wa 2010/11 akiwa ndani ya Azam FC alitupia jumla ya mabao 18 kwa sasa anakipiga na Yanga, timu ya Wananchi.
2011/12
John Bocco, mshambuliaji mzawa aliyetupia zaidi
ya mabao 100, akiwa na Azam FC alitupia jumla ya mabao 19 na kupewa tuzo ya
ufungaji bora katika mabao hayo 19 hakuwa na hat trick mabao mengi aliyofunga
kwenye mchezo mmoja yalikuwa mawili kwenye michezo miwili dhidi ya Yanga na
Coastal Union.
2012/13
2012/13
Kipre Tchetche, nyota huyu alikuwa ni wa miraba minne, nguvu nyingi na akili kumkichwa aliwapa tabu sana mabeki, akiwa na Azam FC alitupia jumla ya mabao 17.
2013/14
Amiss Tambwe, raia wa
Burundi akiwa Simba alitupia jumla ya mabao 19 na alitwaa kiatu cha ufungaji
bora akiwa ndani ya wekundu wa Msimbazi.
2014/15
Simon Msuva, nyota huyu anayekipiga Difaa El Jadida ya Morocco hakuwa na ugomvi na nyavu ila alikuwa anazipa shida kwa sana, akiwa na Yanga alitupia jumla ya mabao 17.
2015/16
2014/15
Simon Msuva, nyota huyu anayekipiga Difaa El Jadida ya Morocco hakuwa na ugomvi na nyavu ila alikuwa anazipa shida kwa sana, akiwa na Yanga alitupia jumla ya mabao 17.
2015/16
Amiss Tambwe arirejea kwenye ubora wake safari hii akiwa na jezi ya Yanga alitupia jumla mabao 21 ndiye aliyejitutumua kupita ile rekodi ya mabao chini ya 20, kwa sasa ametimka mazima Bongo yupo uarabuni akisakata soka la kulipwa.
2016/17
Simon Msuva kwa mara nyingine tena alizidi kuuwasha moto na aliibuka mfungaji bora akiwa na Yanga alitupia jumla ya mabao 14 sawa na Abdulrahman Mussa aliyekuwa akikipiga Ruvu Shooting.
2017/18
Emmanuel Okwi, nyota
huyu raia wa Uganda akiwa na Simba msimu wa 2017/18 aliibuka mfungaji bora
baada ya kutupia jumla ya mabao 20, alikwama kufikia mabao 21 baada ya Juma
Kaseja kuipangua penalti aliyopiga uwanja wa Taifa.
Rekodi zote zilizowekwa nyuma zikavunjwa na Meddie Kagere msimu wa 2018/19 akiwa na Simba alitupia jumla ya mabao 23 rekodi ambayo ilikuwa haijawekwa na wafungaji wengi ndani ya Bongo kuanzia miaka ya 2000.
Rekodi zote zilizowekwa nyuma zikavunjwa na Meddie Kagere msimu wa 2018/19 akiwa na Simba alitupia jumla ya mabao 23 rekodi ambayo ilikuwa haijawekwa na wafungaji wengi ndani ya Bongo kuanzia miaka ya 2000.
0 COMMENTS:
Post a Comment