UONGOZI wa Azam FC
umesema kuwa kichapo cha mabao 5-0 walichoshusha mbele ya GreenWarriors ni
manyunyu tu kuelekea kwenye mchezo wao wa ushindani dhidi ya Simba utakaochezwa
Octoba 23 uwanja wa Uhuru.
Azam FC iliwatumia
wachezaji wake wengi ambao hawajapata nafasi kwa muda ikiwa ni pamoja na nahodha Agrey Moriss
aliyekuwa majeruhi, Seleman Ndikumana na Kassim Khamis ambao walikuwa hawapati
nafasi kikosi cha kwanza.
Akizungumza na Saleh Jembe, Idd Cheche, kocha msaidizi wa Azam FC amesema kuwa ni
hesabu za timu kuzidi kutengama hasa wakati ambao ligi imesimama jambo
litakaloimarisha kikosi kuwa cha ushindani.
“Huu ni mwanzo tu kwani
kwa sasa ligi imesimama na tuna jiaandaa na mchezo wetu dhidi ya Simba, bado
kikosi kinaimarika na tunaamini tutakuwa imara kwenye michezo yetu yote ya ligi
huu ni mwanzo tu,” amesema Cheche.
Mabao ya Azam mbele ya
GreenWarriors uwanja wa Azam Complex yalifungwa na Abdlkassim Khamis alitupia
mawili huku Donald Ngoma,Richard Djod na Seleman Ndikumana wakitupia mojamoja
na leo watakuwa uwanja wa Uhuru kuivaa African Lyon.
Hilo ni tawi la mnyama
ReplyDeleteMnyama anachinjwa hakuna namna!!!!!
Delete