October 14, 2019


SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa leo watamuezi Mwalimu Julius Nyerere kwa vitendo kwa kupambana uwanjani.

Timu ya Taifa leo itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa ulio kwenye kalenda ya FIFA majira ya saa 1:00 usiku nchini Rwanda.

Matola amesema kuwa leo ni siku ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere jambo linalofanya wachezaji kuingia uwanjani wakipambana kupata matokeo chanya ili kumuezi Baba wa Taifa kwa vitendo.

"Wachezaji wanatambua kwamba Taifa leo lipo kwenye kumbukizi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hivyo watapambana kumuenzi kwa vitendo kwa kupata ushindi kikubwa ni sapoti ya wadau na dua," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic