October 14, 2019


Baada ya kucheza na Friends Ranger leo jijini Dar es Salaam, kikosi cha Yanga kinatarajia kucheza mechi yake ya Ligi Kuu iliyokuwa imepigwa kalenda dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.

Mechi hiyo itapigwa Oktoba 22 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini ambayo pia itakuwa sehemu ya maandalizi kuelekea kuwakabili Pyramids FC ya Misri.

Yanga itaanzia nyumbani mechi hiyo kabla ya kurejeana na waarabu hao katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika Novemba 3 mwaka huu.

Kuelekea mechi na Pyramids, Yanga itaweza kuwa na kikosi chenye ongezeko la wachezaji wengine ikiwemo David Molinga na Mustafa Suleiman ambao wapo kwenye mchakato wa kutumiwa vibali vyao kutoka CAF

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic