October 13, 2019


KHE! Kumbe baba wa mshambuliaji wa Taifa Stars na Klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta hakuwa anafahamu chochote kuhusiana na ndoa ya kijana wake huyo.

Samatta alifunga ndoa Oktoba 10, mwaka huu na mzazi mwenzie, Neima Mgange aliyezaa naye watoto wawili ambao ni Karimu ambaye ni wa kiume na wa kike ni Ismini. Ndoa hiyo ilifungwa Mtoni Kijichi jijini Dar kisha kumalizikia Kigamboni.

Mzee Samatta alisema kuwa, mwanaye huyo alimpatia taarifa ya kufunga ndoa yake siku moja kabla ya tukio, hivyo kumfanya akawaombe radhi wazazi wa mwanamke ili mambo yaende huku baadhi ya ndugu wakishindwa kuhudhuria na kutoa lawama za ucheleweshwaji wa taarifa.

“Mbwana alivyofika hapa (kutoka Ubelgiji) alinieleza dhamira yake ya kutaka kuoa siku moja kabla ya tukio hata mimi nilishtuka sana, nikamueleza asione jambo la ndoa ni dogo, ni jambo kubwa linalohitaji maandalizi.

“Hakujali hilo na alishikilia msimamo wake hivyo sikuona sababu ya kumzuia, nikaenda kwa wazazi wenzangu kuomba radhi, niliwasihi sana kwa jambo la kushtukiza, nashukuru Mungu waliweza kunielewa.

“Ndoa ilifungiwa Mtoni Kijichi majira ya saa 2 usiku na ilivyofika saa 4 ikaisha, awali ilikuwa ifungwe mchana lakini ‘kokolo kakala’ (kujiremba) za wanawake ikabidi ifungwe usiku, hivyo nashukuru Mungu kwa sasa Samatta ana mke halali ambaye ni mama watoto wake wawili.

“Tunatarajia kufanya sherehe mwezi ujao atakapokuja katika mechi za makundi ya Afrika ndipo watu wote watapata nafasi ya kusherehekea kwa pamoja, safari hii hata baadhi ya ndugu hawakupata nafasi ya kuhudhuria, hivyo kuna lawama nyingi lakini kitu cha msingi ndoa imepita, katika sherehe watakuwepo,” alisema mzee Samatta.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic