October 20, 2019


Beki Mtanzania anayekipiga katika klabu ya Highlands Park ya Afrika Kusini, Abdi Banda, mpaka sasa hajafanikiwa kucheza mchezo wowote ndani ya timu hiyo.

Katika mechi sita ilizocheza Highlands Park msimu huu ambazo ni sawa na dakika 540, Banda hajabatika kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo ambayo ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.

Banda amesema inahitaji kupambana zaidi ili kupata namba ndani ya kikosi kutokana na kukaa nje kwa muda bila kucheza.

Ameeleza kuwa bado hajawa fiti vizuri, kitu ambacho kinasababisha asiwe sehemu ya kikosi huku akiahidi kujituma mazoezini ili amshawishi kocha wake aweze kumpanga.

"Kwakweli bado sijabahatika kucheza mpaka sasa ukiangalia nilikuwa majeruhi kwa muda mrefu ila nitapambana kwa kadri ya uwezo wangu niweze kucheza.

"Naamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu atanisaidia kurudi dimbani na hii itatokana na jitihada zangu, mpaka sasa timu ishacheza mechi sita na tuko nafasi ya tano tukiwa na alama 11," alisema Banda ambaye aliwahi kuichezea Simba SC.

Katika mechi sita ilizocheza Highlands, timu hiyo imefanikiwa kushinda tatu, sare mbili na ikipoteza mchezo mmoja.

Ikumbukwe Banda alijiondoa katika kikosi cha Taifa Stars hivi karibuni kilichoitwa na Kocha Mrundi, Etienne Ndayiragije kwa ajili ya mechi ya kufuzu CHAN dhidi ya Kenya kutokana na kuwa majeruhi akihofia usalama wake sababu alikuwa bado hajasaini mkataba na Highlands.

1 COMMENTS:

  1. Banda aliitwaje kwenye mechi ya kufuzu CHAN wakati yeye hachezi ligi ya ndani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic