October 20, 2019


LEO saa 12:30 Uwanja wa Old Trafford huko mjini Manchester kutakuwa na bonge moja ya gemu ikiwa ni raundi ya tisa Premier League.

Mahasimu wawili, Manchester United na Liverpool watakuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu.

Liverpool msimu huu amecheza mechi nane na ameshinda zote ana pointi 24 kibindoni akiwa  nafasi ya kwanza huku United ina pointi tisa katika mechi nane alizocheza ameshinda mbili ikiwa nafasi ya 12.

Takwimu zinaonyesha timu hizi zimekutana mara 55 premier League, Manchester United ameshinda mara 28 kati ya hizo 16 akiwa nyumbani huku Liverpool ilishinda mara 14 mara tano ilikuwa Old Trafford.

Jumla ya kadi nyekundu 16 zimetolewa huku United akiwa ameonyeshwa kadi tisa na Liverpool saba.

Kwa upande wa kadi za njano Liverpool ameonyeshwa  86 United wana 100 kwenye jumla ya kadi za njano 186.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic