BODI YA LIGI HAITAKI UTANI KABISA, YATOA ONYO KALI YANGA,
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, ameipa onyo kali Klabu ya Yanga na kuitaka kutoomba tena kusogezwa mbele kwa mchezo wao wowote wa ligi kuu pasipokuwa na sababu za msingi.
Wambura ametoa kauli hiyo baada ya Bodi ya Ligi kukubali ombi la Yanga la kusogeza mbele mchezo wa ligi.
“Tumekubaliana na Yanga juu ya ombi lao na sasa michezo yao yote miwili itachezwa wiki hii, wataanza na Polisi Tanzania Alhamisi, kisha mchezo mwingine watalazimika kucheza tarehe 6 ambayo itakuwa Jumapili dhidi ya Coastal Union.
“Sambamba na hilo, tunatoa onyo kwa Klabu ya Yanga na klabu nyingine yoyote kuacha hii tabia ya kuomba michezo yao isogezwe mbele bila sababu za msingi kwani hii tabia ikiendelea itatuletea mkanganyiko huko mbele,” alisema Wambura.
Yanga walipeleka ombi Bodi ya Ligi ya kutaka mchezo wao na Polisi Tanzania kusogezwa mbele kwa kile walichodai timu yao imeshindwa kuwasili Dar kwa wakati ikitokea Zambia ilikokuwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
simba iliweka viporo 21 mbona hamkutoa onyo bali mlisapoti
ReplyDeletembafuuuuu elewa tamko kazi yako kukarii tumbo wewe
DeleteNyie maboya
ReplyDelete