October 2, 2019


Bahati inamnyookea! Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ amepata shavu la kutangaza madini ya Tanzanite.

Balozi wa Tanzanite nchini, Nangasu Warema alisema kwamba Harmonize atakuwa akiyatangaza madini hayo ndani na nje ya nchi kupitia muziki wake.

“Tumeshaongea na Harmonize na ameahidi kuanza kuyatangaza madini haya ya Tanzanite, hivyo nawaomba Watanzania wote waanze kujisikia fahari na madini haya kwani ni yetu sote,” alisema Warema.

Warema alitoa rai kwa Watanzania kujivunia rasilimali zilizopo nchini kwani Tanzanite ni madini ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee duniani.

“Kikubwa ni kupenda vya kwetu, itakuwa jambo jema kama Watanzania wataanza kuvaa madini haya kama wanavyovaa vitu vya madini mengine.

“Pia kwa watu maarufu nchini niwaombe sana kuanza kuyatangaza madini haya popote mnapokuwa, kwani ni madini pekee yanayopatikana Tanzania tu,” alimaliza kusema Warema.

Warema aliteuliwa na kamati za madini katika kikao cha sita kilichofanyika Tanga mwezi uliopita chini ya Waziri wa Madini, Dotto Biteko.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic