Rais wa Shirikisho la Soka nchini Bulgaria ametangaza kujiuzulu nafasi ya urais kufuatia agizo la Waziri wa Michezo kumtaka afanye hivyo.
Katika mechi ya kufuzu michuano ya Euro 2020 nchini Ujerumani kati ya wenyeji Bulgaria dhidi ya Wageni England iliyochezwa jana kwenye mji wa Sofia nchini Bulgaria, mashabiki wa Bulgaria walikuwa wakiwafanyia vitendo vya kibaguzi.
Ubaguzi huo ulienda kwa wachezaji wenye rangi nyeusi pale wanapopata mpira kwa kuwazomea kwa mtindo wa kulia kama nyani.
Kufuatia tukio hilo ambalo lipigwa vita sana kwenye mchezo wa soka, Waziri wa Michezo nchini Bulgaria, Boyko Borissov, amemtaka rais wa Shirikisho la Soka nchini humo kujiuzulu na rais ametekeleza jambo hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment