October 16, 2019


Ni neema tunaweza kusema zimerejea Yanga kufuatia kurejea kwa wachezaji wake watano waliokuwa majeruhi baada ya kuanza mazoezi mepesi juzi Jumatatu.

Wachezaji hao walianza mazoezi wakiwa wakiwa katika program maalum wakati kikosi cha timu hiyo kikiwa dimbani kucheza dhidi ya Friends Rangers ambayo ililala kwa mabao 4-2.

Mrisho Ngassa, Patrick Sibomana, Paul Godfrey 'Boxer', Lamine Moro na Sadney Urikhob ndiyo wachezaji waliokuwa wakifanya mazoezi hayo wakati mechi inaendelea.

Kurejea kwa wachezaji hao kumeanza kutia morali kwa Yanga ambayo itakabiliana na Pyramids FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Oktoba 27 mwaka huu.

Yanga itakipiga na waarabu hao kutoka Misri ambapo mechi ya raundi ya kwanza itafanyika jijini Mwanza kwenye Uwanja wa CCm Kirumba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic