DAVID MOYES ATUMA MAAGIZO YA KIBABE MAN UNITED
Kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes ameishauri klabu hiyo kutouza mastaa wake na kufanya wanavyoweza kuendelea kubaki na Paul Pogba.
Pogba amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo huku akiwaniwa kwa ukaribu na Real Madrid baada ya kunukuliwa kuwa anatamani kupata changamoto mpya.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, hivi karibuni alikutana na kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane alipokuwa mapumzikoni Dubai na haikujulikana walizungumza kuhusu nini.
Moyes, ambaye aliinoa United msimu wa 2013/14 amesema kumpoteza staa huyo ni mwanzo mbaya wa kupoteza nguvu ya ushawishi kwenye soka na jambo la muhimu ni kuhakikisha nyota wote wakubwa wanaendelea kubaki klabuni kwa gharama yoyote.
“Pogba bado ni kiungo bora wa timu, anao uwezo wa kucheza timu yoyote Ulaya. Kwa hadhi yake anatakiwa kuwa mtu ambaye anaonyesha utofauti lakini hafanyi hivyo mara zote, pamoja na hivyo bado naamini anatakiwa kuendelea kubaki,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment