KOCHA MANCHESTER APEWA SHARTI LA KUMSAJILI MCHEZAJI HUYU PALE ENGLAND, KISA ...
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes anaaamini timu hiyo inayosuasua kwa sasa
wanaweza wakafaidika wakimsajili Mesut Ozil kuongeza ubunifu katika safu ya mashambulizi ambayo imepwaya.
United imepata ushindi wa bao moja ugenini baada ya kipindi cha miezi saba hapo jana katika mchezo
wa Europe Ligue dhidi ya Partizan mjini Belgrade.
Vijana hao wa Ole Gunnar Solskjaer walionyesha kiwango dhaifu, ashukuriwe Anthony Martial ambaye
aliipatia goli la penati katika mchezo huo.
Kwa kipindi hiki magoli yamekuwa adimu kufungwa na Man United, ambapo katika mechi nane zilizopita za Premier Ligue ni magoli sita tu yamefungwa, ikumbukwe mechi yao ya kwanza ligi waliondoka na ushindi wa 4 – 0 dhidi ya Chelsea.
Je, Mesut Ozil ambaye kwa sasa hachezeshwi Arsenal, atakuwa ni suluhisho? “Man United ingekuwa na mchezaji kama Ozil ambaye anaunganisha timu kwa pamoja,” Scholes aliiambia BT Sport kufuatia ushindi huo wa timu yake ya zamani.
“[Yeye ni] mchezaji anayeweza kuunganisha timu kwa pamoja. Ana ubora sana, ameonesha hilo”
“Atakuwa ni jibu katika kipindi kifupi, sijui. Nafikiri hayo yapo juu yake.”
“Siwezi [kuona inatokea], lakini ni aina ya mchezaji Man United wafanye nae kazi kwa kipindi kifupi.
Ozil jana hakuwepo katika mchezo wa Europe Ligue kati ya Arsenal dhidi ya Vitoria katika uwanja wa
Emirates.
Mchezaji huyo mstaafu wa kimataifa wa Ujerumani, mechi yake ya mwisho ya ushindani kuwepo ni
ilikuwa Septemba 24 ambapo walipata ushindi wa 5 – 0 dhidi ya Nottingham Forest katika kombe la
Carabao, ikumbukwe Ozil amecheza mechi moja ya Premier Ligue katika msimu huu 2019 – 2020.
Kuna taarifa zinasema Ozil hana jitihada katika mazoezi na ndio maana anawekwa benchi, ingawa kocha
wa Arsenal ‘Unai Emery’ amekanusha taarifa hizo za uongo.
“Mesut Ozil, kwa sisi, ni muhimu. Kuna muda mchezaji anakuwa ana umuhimu kucheza, kukaa benchi au kujiandaa kucheza mechi ijayo,” aliwaambia waandishi.
“Hii ndio fikra yetu na ndio njia tunayotaka kuiunda kwa wachezaji wetu 25 katika timu. Ozil yupo katika njia sawia na nakuambia katika kipindi cha miezi mitatu sasa anajituma na
anaendelea vizuri katika mazoezi. Kama tunamuhitaji tutamtumia.”
0 COMMENTS:
Post a Comment