EXCLUSIVE: YANGA KUENDELEA KUWAKOSA FALCAO NA MUSTAFA, MWAKALEBELA AFUNGUKA
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela, amesema wachezaji David Molinga 'Falcao' na Mustafa Suleiman hawatatumika katika mchezo dhidi ya Pyramids katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga itakuwa na kibarua cha raundi ya kwanza dhidi ya Pyramids kutoka Misri Oktoba 27, mechi itayaochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana, Mwakalebela amesema wachezaji hao hawatweza kutumika sababu ya kukosa vibali kutoka CAF.
Ameeleza kuwa wataweza kutumika endapo timu itangia katika hatua ya makundi na katika michezo ya Ligi Kuu Bara wataendelea na kazi kama kawaida.
Tangu michuano ya kimataifa ianze, wachezaji hao hawajashiriki mashindano hayo sababu ya kukosa vibali.
Kusema ukweli viingilio ni vya juu sana angalau wangefanya kima cha chini 5,000 cha juu 50,000 lengo lisiwe mapato bali liwe ni kuujaza uwanja sasa sidhani kama kwa viingilio hivyo mtaujaza uwanja KWANI HII MECHI NI YA MUHIMU SANA KWA MAANA NYINGINE NAFASI NI MOJA TU KUSHINDA MECHI HII YA NYUMBANI HAKUNA NAFASI NYINGINE MSIFIKIRIE KWENDA MISRI KUSHINDA....USHINDI WENU NI KUUTUMIA UWANJA NA KUHAMASISHA MCHEZAJI NO. 12 AINGIE KUTOA HAMASA NA USHANGILIAJI. Halafu suala la vibali vya CAF watu wanachanganywa mlisema mmepokea barua ikiwaruhusu kuwatumia leo mnasema kanuni...sasa kwanini mliwapa matumaini watu kuwa watatumika halafu leo mmeyazima matumaini hayo?
ReplyDeleteHawajitambui hao viongozi
ReplyDelete