October 18, 2019


OBREY Chirwa mshambuliaji wa Azam FC, leo ameongoza kikosi chake cha Azam FC kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Transit Camp mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Chamazi.

Azam FC iliyo chini ya Idd Cheche ambaye ni Kocha Msaidizi kwa sasa inaendelea na maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Simba utakaopigwa Octoba 23 uwanja wa Uhuru.

Mabao mengine mawili ya Azam FC yalipachikwa na kiungo mshambuliaji mwenye makeke uwanjani Richard Djod.

Huu ni mchezo wa tatu kwa Azam FC wa kirafiki kucheza na kushinda walianza na Green Warriors Azam FC ilishinda mabao 3-0 ikashinda mabao 2-0 dhidi ya African Lyon na leo imemalizana na Transit Camp.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic