October 12, 2019


Kikosi cha Simba kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bandari FC ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bao pekee la mechi hiyo lilifungwa na Ibrahim Ajibu katika dakika ya 77 kipindi cha pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Rashid Juma.

Katika mchezo huo, Simba walikuwa na ufundi mwingi haswa katika kukontro mipira kuelekea katika lango la wapinzani ingawa mingi haikuwa na macho katika lango la Bandari.

Aidha, kipa Beno Kakolanya aliibuka shujaa baada ya kuokoa mashuti mengi kutoka wa wapinzani.


1 COMMENTS:

  1. Tumemuona Ibrahim Ajibu hakika ameonesha kuwa amepevuka sasa sijui kama atadumisha au kuzidisha bidii nakuwa bora zaidi kwani vijana wetu ni kama maji ya bahari kujaa na kuondoka.Binafsi katika mechi hii ya Simba na bandari nimefurahishwa na wale wachezaji wenye Simba yao wameonekana kuimarika. Nikisema wachezaji wenye Simba yao ninamaana na wale vijana waliolelewa pale simba kwa madhumuni ya kuja kuishibisha Simba na wachezaji wazalendo wenye mapenzi na timu. Ajibu,Shamte,Ndemla,Rashid Juma na wengine vijana kadhaa ndani ya Simba nadhani ni wakati wao wa kuiteka Simba nakuwa ndio muhimlili wa timu wenzetu warabu wa kaskazini mara nyingi hutuzidi hapa.Timu zao mara nyingi hujengwa na wachezaji wengi wazawa wenye uchungu na uwezo ndani ya tmu zao na kama watajaliza wageni wanakuwa wawili watatu lakini wenye uwezo wa kweli kweli. Upo uwezekano kabisa wa Simba kurudi kimataifa mwakani ni vyema vijana hawa wakapigana na kuitumia ligi kuu kujijenga wakilenga michuano ya kimataifa mwakani kwani ukiangalia kwa undani zaidi kuondolewa kwa Simba mapema kimataifa mara hii ni kule kutegemea wachezaji wageni amabao wengi wao hawakuwa tayari kutokana na upya na kadhalika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic