UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hautakuwa na cha msalia mtume mbele ya Pyramids kwenye mchezo wao wa hatua ya mtoano utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Yanga itamenyana na Pyramids Octoba 27 kabla ya kurudiana nao nchini Misri.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wana uhakika na kile wanachokifanya kwa sasa jambo linalowapa kujiamini.
"Tunajua utakuwa ni mchezo mgumu ila hakuna namna ni lazima tupambane kupata matokeo, tunaamini katika hilo, mashabiki watupe sapoti lengo leu ni kusonga mbele kimataifa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment