October 12, 2019



Full Time: Simba SC 1-0 Bandari FC

Dak ya 90+4, faulo kuelekea Bandari, anapiga Ajibu, piga pale, inagonga nyavu za nje.

Dak ya 71, Goooli, Ajibu amefunga bao la kwanza kwa Simba baada ya pasi nzuri kutoka kwa Rashid Juma.
Dak ya 73, ufundi mwingi unaoneshwa hapa na pale kwa timu zote mbili, tatizo limekuwa gumu kwenye kufunga.
Dak ya 67, Wawa anapewa kadi ya njano.
Dak ya 66, Juma anaingia na maajabu yake, anapiga shuti kali lakini linapanguliwa na kipa wa Bandari.
Dak ya 65, Kanda anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Rashid Juma.

Dak ya 63, Mlipili ambaye ameingia kipindi cha pili anakokota gozi kuelekea mbele,
Dak ya 57, Simba wamekuwa wakitengeneza nafasi nzuri, bado tatizo ni umaliziaji, halikadhalika kwa Bandari FC.
Dak ya 50, Kahaaata, piga shuti moja kali lakini Wantika anaipangua na kuitoa nje, inakuwa kona
Dak ya 48, Kahata anammegea vizuri Shiboubm anaoiga krosi juu inatoka nje.
Dak ya 46, kipindi cha pili kimeanza


Mapumziko, Simba SC 0-0 Bandari FC

Dak ya 45, zimeongezwa dakika mbili kuelekea mapumziko.
Dak ya 41, bado ngoma ni ngumu kwa timu zote mbili, hadi sasa ni 0-0.
Dak ya 40, Ajibu anashindwa kucheka na nyavu akiwa kwenye nafasi nzuri, kipa Wantika anaudaka mpira.
Dak ya 39, William anapiga shuti moja kali, kipa Kakolanya anapangua na inakuwa kona.

Dak ya 36, Bandari wanatengeneza nafasi nyingine lakini inakuwa haina macho, Kocha Be Mwalala anaonekana kulalama juu ya wachezaji wake.
Dak ya 33, Tairone anapewa kadi ya njano kwa kucheza madhambi.
Dak ya 31, William Wadri wa Bandari amedondoka chini, Mwamuzi Herry Sasii amesimamisha mpira.
Dak ya 27, Wilkeeeeeeer, piga moja juu inaenda juu ya lango, ni baada ya kutengewa pande zuri na Shiboub.
Dak ya 25, Simba wanapasiana tena nje kidogo ya eneo la hatari la Bandari, kuipenya ngome yao imekuwa si kazi rahisi.
Dak ya 24, Bandari wanatoa tena mpira nje, Simba wanarusha.
Dak ya 22, Simba wanapanda tena, kwake Wilker, anapasia gozi kwa Fraga, kwake Shiboub, Bandari wanauchukua.

Dak ya 20, Mpira unarushwa kuelekea Bandari FC
Dak ya 18, Shiboub anafanyiwa madhambi, ni faulo kuelekea Bandari.
Dak ya 17, Simba wanajitahidi kutengeneza mashambulizi lakini umakini katika kumalizia ni tatizo.
Dak ya 16, William anapiga tena, Simba wanaokoa.
Dak ya 15, Bandari wanapata kona ya kwanza, anakwenda kupiga William, piga pale inakuwa kona tena, Kahata ametoa,
Dak ya 13, Ni golikiki kuelekea Simba, Bandari wanacheza.

Dak ya 12, mpira umetoka, unarushwa kuelekea Simba
Dak ya 10, Simba wanafanya shambulizi lingine, wanapasiana kuelekea katika lango la Bandari vizuri, mpira unamkuta Shiboub, anapiga shuti dhaifu na kipa wa Bandari anadaka.
Dak ya 8, Bandari wanafanya shambulizi moja kali lakini linashindwa kuzaa matunda, inakuwa golikiki.
Dak ya 6, Simba wanapiga gonga nyingi karbu na eneo la hatari la Bandari lakini wanashindwa kuwa na namna nzuri ya kupenya.
Dak ya 3, mechi imeanza katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic