KANDA AINGIWA NA HOFU SIMBA
Licha ya Simba kuibuka na ushindi katika mechi nne mfululizo za Ligi Kuu Bara, straika Mkongomani wa Simba, Deo Kanda, amesema ligi ya Bongo inahitaji juhudi kubwa za kupambana sababu ni ngumu.
Kanda aliyesajiliwa na Simba akitokea TP Mazembe inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo, mpaka sasa hajafanikiwa kuitendea jezi yake namba 07 iliyokuwa inavaliwa na Emmanuel Okwi ambaye alitimkia uarabuni.
Kanda ameeleza kuwa kwa ligi ya Tanzania inamhitaji kupambana vya kutosha ili kutimiza kile kinachohitajika.
"Tumeshinda mechi zote lakini nimegundua kuwa ligi ya hapa ni ngumu.
"Inahitaji bidii sana kwa mchezaji kuweza kufanya vizuri, bila hivyo inakuwa ngumu.
"Licha ya ugumu, Simba ni timu nzuri ambayo wachezaji wake wanajitolea kwa juhudi, nahitaji kuweka zaidi bidii ili kuweza kufika mbali maana kila tunayokutana nayo inakuwa imejipanga", alisema.
uko sahihi na hata kiwango bado licha ya kushinda
ReplyDelete