SHEVA AFUNIKA KWA USAJILI WA MAMILIONI SIMBA
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Miraji Athumani 'Sheva' ameingia kwenye rekodi ya ajabu ndani ya tmu hiyo kwa kusajiliwa kwa kiasi kidogo cha fedha tofauti na mastaa waliopo ndani ya timu.
Sheva alijiunga na Simba akitokea Lipuli kwa shilingi za kitanzania ambazo ni milioni 20 tu.
Nyita huyo tangu atue Simba amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi akiichezea timu yake michezo mitano ya mashindano ambapo minne ni ya Ligi Kuu na mmoja wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sheva ameisababishia Simba mabao mawili ya penati ikiwa ni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo kwenye Uwanja wa taifa, pia mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Mbali na hilo, Sheva amefanikiwa kutengeneza bao moja katika mechi ya ligi dhidi ya Biashara United
Wachezaji waliosajiliwa kwa bei zilizo juu yake msimu huu ni Beno Kakolanya (mil 50), Ibrahim Ajibu (mil 80, Deo Kanda (mil 100), Kennedy Juma (mil 30), Wilker da Silva na Tairone do Santos na Gerson Fraga ambao wote ni wabrazil waliogharimu milioni 70.
Wewe mwandishi shika adabu yako acheni upumbavu. Milioni mia nane mnazodai kasajiliwa Ajibu mnazijua au mnaropokwa tu kama vile mmetumia kilevi kikali.
ReplyDelete80 bwana
Delete