KENYA NI BALAA, MWANARIADHA MWINGINE AVUNJA REKODI YA DUNIA
Mwanariadha kutoka nchini Kenya, Brigid Kosgei amevunja rekodi kwenye mbio za Chicago Marathon za wanawake duniani ameibuka na kubaki katika nafasi yake ya kwanza.
Brigid Kosgei mwenye miaka 25, Ameweka rekodi ya kumaliza mbio kwa 2:14: 04 akivunja rekodi iliyokuwepo kwa dakika moja na Sekunde 21, ambapo bado anakuwa amevunja rekodi ya Radcliffe ambaye alishinda katika 2:15:25 katika mashindano ya mbio ya mwaka 2003.
Msichana huyo ameshangaza wengi katika ushindi alioupatia nchi yake na kuwa mshindi mdogo zaidi wa mashindano.
Mshindi aliyefuata ametokea Ethiopa’s Ababel Yeshaneh, ndio mshindi wa pili wa mashindano ya mbio ya Chicago na alishinda katika dakika ya 6 na sekunde 47.
Chicago marathon ni miongoni mwa mashindano ya mbio zinazotambuliwa rasmi na shirikisho la riadha duniani IAAF.
0 COMMENTS:
Post a Comment