October 14, 2019


Kikosi cha Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Friends Rangers katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Chuo cha Polisi, jijini Dar es Salaam.

Alikuwa ni Maybin Kalengo aliyeanza kucheka na nyavu za Rangers mnamo dakika ya 23 kipindi cha kwanza kabla ya David Molinga 'Falcao' kuingia kambani mara mbili katika dakika za 24 na 27 kipindi cha kwanza na kuifanya Yanga ifikishe mabao matatu.

Haikushia hapo, Yanga waliendelea moto kwa kuongeza bao la nne lililofungwa na Papy Tshishimbi kwenye dakika ya 32.

Hadi kufikia kipindi cha kwanza kinamalzika, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 4-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Rangers wakionekana kuja juu wakitaka kusawazisha ambapo walifanikiwa kuingia kambani mara mbili na kuufanya mchezo umalizike kwa mabao 4-2.

Baada ya mechi hii ya leo, Yanga sasa sasa watakuwa wanajiandaa na safari kuelekea Mwanza ambapo wataweka kambi maalum kabla ya kukutana na Pyramids katika Kombe la Shirikisho Afrika.






5 COMMENTS:

  1. 4-3 lakini blog hii inadanganya ili kufanya matokeo yaonekane Yanga imeshinda kwa kushinda.Tofauti ni goli moja tu.Semeni kweli.

    ReplyDelete
  2. Mwarabu anatetemeka!Friends Rangers kafungwa 4-3 na Yanga. Hii blogu inachekesha. Kweli kuwafunga Friends Rangers kuwe salamu kwa waarabu?

    ReplyDelete
  3. Beki nayo iangaliwe kwa makini, magoli matatu kambani kipindi cha pili?! Bado timu inasheki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic