ETIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo mbele ya Ndanda FC utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex leo saa 1.00 usiku.
Ndayiragije amesema kuwa anatambua ugumu wa ligi pamoja na ushindani ulivyo ila hana mashaka na kikosi chake kupata matokeo.
"Natambua kwamba ligi ni ngumu na kila timu inahitaji pointi tatu hilo halinipi mashaka kwa kuwa naamini uwezo wa wachezaji wangu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema.
Huu unakuwa mchezo wake wa kwanza kucheza nyumbani baada ya kufungua ligi kwa ushindi wa bao moja dhidi ya KMC ugenini, uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment