MABONDIA wa
ngumi za kulipwa nchini, Issa Nampepeche na Ally Hamisi wanatarajia kupima
uzito kesho tayari kwa pambano la usiku wa mabingwa litakalofanyika Oktoba 4,
mwaka huu kwenye Ukumbi wa Club 361 uliopo Mwenge, Dar.
Mbali
ya mabondia hao wengine watakaopima uzito kwa ajili ya pambano hilo ni Said Sudi atakayezichapa na Maganga Kulwa,
Ibrahim Makubi dhidi ya Abdallah Kingolwira, Hashimu Msungo vs Epson
Lewis wakati Salumu Omari atamalizana na Ramadhani Chicho huku
yakiwa chini ya udhamini wa Gazeti la Championi, +255 Global radio,
Smart Gin, Glady Matata na Kiwango Security.
Akizungumza
na Championi Jumatano, mratibu wa pambano hilo, Seleman Semunyu alisema kuwa
maandalizi ya kuelekea katika pambano hilo yamekamilika ambapo kesho mabondia
wanatarajia kupima uzito kwenye Ukumbi wa Club 361.
“Maandalizi yanakwenda vizuri kwa mabondia
wote ambao watapanda ulingoni siku hiyo ambayo itakuwa ni kazi moja tu ya
kuwapongeza mabondia wetu ambao wamechukua mikanda ya ubingwa nje ya mipaka ya
Tanzania.
“Uzito tumepanga wapime kesho Alhamis kabla ya siku ya Ijumaa ambayo mabondia wenyewe ndiyo watapanda ulingoni, kikubwa mashabiki wa mchezo wa ngumi za kulipwa wajitokeze kwa wingi siku hiyo kushuhudia ngumi zikifanyika katika ustarabu wa hali ya juu kwa kiingilio kidogo,” alisema Semunyu.
0 COMMENTS:
Post a Comment