KIMENUKA!! YANGA WATAKA ZAHERA AFUTWE KAZI - VIDEO
Baada ya kupoteza mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika jana dhidi ya Pyramids FC kutoka Misri kwa mabao 2-1, baadhi ya mashabiki wa Yanga wameutaka uongozi wa timu hiyo kuachana na Zahera na badala yake atafutwe kocha mwingine.
MABADILIKO YA UENDESHAJI NA KUINGIA KWENYE UWEKEZAJI HAYAEPUKIKI HATA KAMA TIMU NI YA WANANCHI
ReplyDeleteBaada ya michezo kadhaa ya kimataifa na ligi picha halisi inaonekana jinsi timu isivyobadilika na kuwaudhi mashabiki wake.
Kama nilivyoshauri huko nyuma rejea baadhi ya maandiko yangu.
Nadhani ni wakati sahihi kukaribisha muundo mpya wa uwekezaji na uendeshaji wa timu ya soka ya Yanga...mpira ni pesa matokeo mazuri ya uwanjani yanachangiwa na vinasaba vingi....kimojawapo ni kuwekeza kwenye benchi la ufundi bora na kusajili wachezaji bora huu ndio wakati muafaka wa Yanga kufanya mabadiliko wakati ligi haijafikia nusu...maeneo matatu
1. Uwekezaji na Muundo wa Uendeshaji wa Kisasa
2. Kulifumua Benchi la Ufundi
3. Kuongeza wachezaji mahiri na kupunguza wachezaji wasio na tija..
Tatizo ni kwamba hakuna dalili ya mabadiliko ya kiuchezaji, kimfumo, kiufundi na kimbinu kwa timu nzima wachezaji wamesajiliwa na Kocha mwenyewe sasa ni nani wa kubeba lawama kama si kocha na wasaidizi wake pamoja na wachezaji?? Wafadhili wamefanya sehemu yao viongozi wanafanya sehemu yao ingawa wako very slow (uwekezaji na kufanya mabadiliko ya kiundeshaji) viwanja na miundo mbinu...ni wakati wa kufanya vitendo sasa na kufanya maamuzi magumu....ili kunusuru shari...mashabiki wanajitolea sana, wanahamasishana sana na wanaichangia timu yao ingawa ni buku....lakini kwakweli wanaangushwa na matokeo ya uwanjanI...mtaani wanachekwa na kusimangwa mno kwa hiyo wanapodai Kocha Aondolewe wana haki ya msingi kufanya hivyo...ingawa mchezo wa soka una matokeo ya aina 3....tathmini inaoonyesha hakuna improvement kiuchezaji na ndio sababu ya wao kulalamika na kunung'unika na kupaza sauti kutaka Makocha wondolewe....au kulazimisha mabadiliko
Ahsanteni
Good umenena vema, timu haina kocha wala washambuliaji bora hata Mbao FC inajitahidi kuliko Yanga, Yanga siyo timu ya wachezaji kuja kujifunzia, Kocha alisajili mwenyewe na alisema mahitaji yake kwa 100% yamezingatiwa.
Deletenashangaa baada ya mchezo na zesco kisha kurudi Yanga walicheza mechi moja ligi kuu..Kisha katika kipindi ambacho Simba alikamilisha mechi tatu za kirafiki Yanga ilikuwa haijacheza hata mechi moja angalau ya kirafiki.Na Zahera alikuwa hayupo..Utashindaje bila maandalizi hata ukihamishia uwanja wa nyumbani kwenu
ReplyDelete