Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa na kazi ya kupindua meza mbele ya wapinzani wao Pyramids FC nchini Misri kwenye mchezo wa marudio utakaopigwa baada ya wiki mbili.
Ushindi wa mabao 2-1 walioupata wapinzani wao umeongeza uzito kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa leo uwanja wa CCM Kirumba.
Mchezo wa jana Oktoba 27 ulioanza kwa kasi, Yanga ilikubali kwenda mapumziko ikiwa imefungwa bao 1-0.
Kipindi cha pili walianza kwa kasi bado mambo yalikuwa magumu kwa Yanga na kuwapa nafasi wapinzani wao kuandika bao la pili.
Mabadiliko ya kumtoa Mrisho Ngassa nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke pamoja na Juma Balinya kuingia akichukua nafasi ya Makame yaliongeza nguvu kwa Yanga
Iliwachukua Yanga dakika 90 kuandika bao la kwanza kupitia kwa Papy Tshishimbi kwa shuti kali akimalizia pasi ya Kaseke.
Ili kusonga mbele Yanga itatakiwa kushinda mabao 2 ugenini na wanatakiwa kulinda lango lao lisitikiswe na wapinzani.
Itamkosa bekikisiki, Kelvin Yondan ambaye ameonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na kadi mbili za njano.
MABADILIKO YA UENDESHAJI NA KUINGIA KWENYE UWEKEZAJI HAYAEPUKIKI HATA KAMA TIMU NI YA WANANCHI
ReplyDeleteBaada ya michezo kadhaa ya kimataifa na ligi picha halisi inaonekana jinsi timu isivyobadilika na kuwaudhi mashabiki wake.
Kama nilivyoshauri huko nyuma rejea baadhi ya maandiko yangu.
Nadhani ni wakati sahihi kukaribisha muundo mpya wa uwekezaji na uendeshaji wa timu ya soka ya Yanga...mpira ni pesa matokeo mazuri ya uwanjani yanachangiwa na vinasaba vingi....kimojawapo ni kuwekeza kwenye benchi la ufundi bora na kusajili wachezaji bora huu ndio wakati muafaka wa Yanga kufanya mabadiliko wakati ligi haijafikia nusu...maeneo matatu
1. Uwekezaji na Muundo wa Uendeshaji wa Kisasa
2. Kulifumua Benchi la Ufundi
3. Kuongeza wachezaji mahiri na kupunguza wachezaji wasio na tija..
Tatizo ni kwamba hakuna dalili ya mabadiliko ya kiuchezaji, kimfumo, kiufundi na kimbinu kwa timu nzima wachezaji wamesajiliwa na Kocha mwenyewe sasa ni nani wa kubeba lawama kama si kocha na wasaidizi wake pamoja na wachezaji?? Wafadhili wamefanya sehemu yao viongozi wanafanya sehemu yao ingawa wako very slow (uwekezaji na kufanya mabadiliko ya kiundeshaji) viwanja na miundo mbinu...ni wakati wa kufanya vitendo sasa na kufanya maamuzi magumu....ili kunusuru shari...mashabiki wanajitolea sana, wanahamasishana sana na wanaichangia timu yao ingawa ni buku....lakini kwakweli wanaangushwa na matokeo ya uwanjanI...mtaani wanachekwa na kusimangwa mno kwa hiyo wanapodai Kocha Aondolewe wana haki ya msingi kufanya hivyo...ingawa mchezo wa soka una matokeo ya aina 3....tathmini inaoonyesha hakuna improvement kiuchezaji na ndio sababu ya wao kulalamika na kunung'unika na kupaza sauti kutaka Makocha wondolewe....au kulazimisha mabadiliko
Ahsanteni