October 25, 2019


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ameahirisha kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa klubu ya Simba Evans Aveva na aliyekuwa makamu wa wake Godfrey Nyange kutokana na hakimu anayesikiliza shauri hilo kupata udhuru.

Wakili wa Serikali Mkuu, Shedrack Kimaro amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya maamuzi na wapo tayari kusikiliza.

Hakimu Ally amesema Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayeendesha kesi hiyo amepata udhuru hivyo anaihairisha shauri hilo hadi tarehe nyingine.

Ally ameahirisha shauri hilo hadi Novemba 5 mwaka huu litakpokuja kwa ajili ya uamuzi. Katika kesi hiyo, washitakiwa hao walikuwa wakikabiliwaa na mashitaka tisa ambapo Septemba 19, mahakama hiyo iliwaondolea mashtaka mawili ya utakatishaji fedha kwakuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuyathibitisha.

Mahakma ilitoa masharti ya dhamana kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao walitakiwa kusaini bondi ya shilingi mil 30, kila mmoja.

Hata hivyo, Mahakama hiyo iliawakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka saba ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo, na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic