KISA LIVERPOOL, SAMATTA APOTEZEA FUNGATE
Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amelazimika kumuacha mke wake Dar, siku chache baada ya ndoa kutokana na kuwahi mechi dhidi ya Liverpool ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Genk itakutana nao Oktoba 18.
Samatta amefunga ndoa na mzazi mwenzie Neima Mgange aliyezaa nae watoto wawili (wakike na kiume), katika ndoa iliyofanyika Mtoni Kijichi jijini Dar huku ikihudhuriwa na watu wachache.
Akizungumza na Spoti Xtra,Baba Mzazi wa Samatta, Mzee Ally Samatta amesema kuwa atalazimika kuunganisha safari baada ya kumaliza mechi ya Taifa Stars kesho nchini Rwanda.
“Samatta amejiunga na timu ya taifa kujiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda kwa kuwa yeye ni nahodha, hivyo akimaliza mchezo huo ataunganisha huko huko Rwanda kuelekea Ubelgiji kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool.
“Kuhusu fungate watapanga weneyewe siku yeyote na kuamua watakwenda kulia wapi kwa sasa wamekosa muda kutokana na majukumu ya kikazi, akirudi mwezi wa 11 ndio mambo mengine yataendelea,” alisema mzee Samatta.
0 COMMENTS:
Post a Comment